MIMBA YA PENNY NA DIAMOND YATOKA
TAARIFA  ya ndani 
zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa  Bongo  Fleva, 
Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka   
zimevuja....
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi   
wanavyodhani.
 
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani  hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo  hicho. 
Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali
   alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na   
ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya kupata habari hizo, mwandishig wetu alilimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Penny: Pole ya nini sasa?
Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine? 
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
 
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine? 
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

No comments:
Post a Comment