RAIS OBAMA ANAELEKEA AFRIKA KUSINI
RAIS wa Marekani Barack Obama leo
Ijumaa anaelekea Afrika Kusini ambapo miongoni mwa shughuli zake atazuru
kisiwa cha Robben Island alikozuiliwa jela rais wa zamani Nelson
Mandela kwa miaka 27.
Rais Obama anakwenda nchini humo
wakati Mandela akiwa katika hali mbaya ya afya. Rais huyo wa zamani
anatibiwa katika hospitali moja ya Pretoria.
Alihamis rais Obama alisema ziara yake
katika eneo ambalo watumwa wa Afrika waliondoka barani humo kwenda
Amerika kaskazini imempa hamasa mpya ya kulinda haki za binadamu.
Obama alitembelea kisiwa cha Goree
kwenye ufukwe wa Senegal Alhamis. Wanahistoria wanasema maelfu ya
Waafrika wanaume kwa wanawake wakiwa wamefungwa minyororo walishikiliwa
huko na kupitia kile kilichoitwa mlango wa kutorudi tena kupanda meli ya watumwa wakielekea bahari ya Atlantic.
Rais Obama alisema ziara yake katika
kisiwa hicho ilimpa hisia kali na nafasi ya kutathmini upya biashara ya
utumwa katika karne ya 16 na 19. Chanzo: Voaswahili
No comments:
Post a Comment