Fernando Torres
MABINGWA wa dunia, Hispania wametinga 
Nusu Fainali ya Kombe la Mabara kufuatia ushindi wa mabao wa 3-0 dhidi 
ya Nigeria usiku huu.
            
Bao maridadi la juhudi binafsi za 
Jordi Alba, mmoja kati ya wachezaji wanane wa Barcelona kwenye kikosi 
cha kwanza cha Hispania, liliiweka Hispania mbele mbele baada ya dakika 
tatu, kabla ya Fernando Torres kufunga bao lake la tano kwenye 
mashindano haya dakika ya 62 kwa kichwa cha mkizi, dakika tatu tu 
aingine aingie kuchukua nafasi ya Roberto Soldado.
Pamoja na kufungwa, Super Eagles walicheza vizuri na kilichowagharimu ni umaliziaji mbovu. Alba akafunga bao la tatu kwa Hispani na la pili kwake katika mchezo huo dakika ya 88.
Matokeo hayo yanaifanya Hispania iongoze Kundi B kwa pointi zake tisa na itakutana na Italia waliowachapa 4-0 katika fainali ya mwaka jana ya Euro 2012 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mabara Alhamisi mjini Fortaleza.
Katika Nusu Fainali nyingine Uruguay iliyoifunga 8-0 Tahiti usiku huu, imeshika nafasi ya pili kwenye Kundi hilo na itamenyana na Brazil katika Nusu Fainali. Nigeria baada ya kufungwa imemaliza katika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu ilizovuna kwa vibonde Tahiti. Chanzo: Binzubeiry
                    
No comments:
Post a Comment