MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUFANYA NGONO NA BINTI WA MOROCCO
Berlusconi
ni mmiliki wa AC Milan, hapa akiwa katika picha ya pamoja na kocha wa
zamani wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti mwaka 2007
Binti wa Morocco, Karima El Mahroug
Rais wa Mahakama, Giulia Turri (katikati) akisoma hukumu
Mwanasheria wa Silvio Berlusconi, Niccolo Ghedini akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama.
MMILIKI wa AC Milan, Silvio Berlusconi
amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kufungiwa maisha kufanya
kazi katika ofisi za umma baada ya kukutwa na hatia ya kumlipa binti
mdogo afanye naye ngono katika moja ya pati zake za 'bunga bunga'.
Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Italia,
Berlusconi, mwenye umri wa miaka 76, alimlipa binti mdogo wa
Morocco, Karima El Mahroug, anayekwenda kwa jina la utani, Ruby, kwa
ajili ya ngono na baadaye akajaribu kumbambikizia kesi ya wizi kwa
kuwapigia simu Polisi na binti huyo akakamatwa. Berlusconi na mwanamke
huyo wamekanusha kufanya ngono.
Mwendesha mashitaka alipendekeza afungwe
miaka sita kwa kuzini ni binti mdogo na matumizi ya nguvu, lakini
majaji watatu wa kike katika Mahakama ya Jijini Milan jana walitaka
afungwe muda mrefu zaidi, miaka saba.
Berlusconi pia amefungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya Waziri huyo Mkuu wa zamani kukutwa na hatia leo.
Lakini mfungwa huyo anaweza kukata rufaa mara mbili kabla hajamaliza kifungo chake, ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka.
Maana yake hatatumikia kifungo chake hadi ashindwe rufaa zake.
Klabu yake ya AC Milan - ambayo
amekuwa Rais wake kwa vipindi vitatu tofauti tangu mwaka 1987 -
inayoundwa na nyota kadhaa akiwemo Mario Balotelli - ilimaliza katika
nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu uliopita
ikizidiwa pointi 15 nyuma ya wapinzani, Juventus.
Baada ya hukumu, Mwanasheria wa
Berlusconi, Niccolo Ghedini, mara moja alitangaza kukata rufaa akisema
hukumu hiyo ni kama ilivyotarajiwa, haikutenda haki.
"Hii ni kinyume cha uhalisia," Ghedini
aliwaambia Waandishi wa Habari nje ya Mahakama. "Nimetulia kwa sababu
nimekuwa nikisema kwa miaka mitatu kwamba kesi haiwezi kuendeshwa hapa,"
alisema Ghedini.
Kimwana: Karima el-Mahroug anafahamika kama 'Ruby the Heartbreaker'
Alisema pati hiyo ya chakula cha usiku
ilikuwa kwa ajili ya watu maaum; Mwendesha mashitaka amesema walifanya
ngono na mwanamke huyo aliyelipwa kuhudhuria.
Hata kama Berlusconi alikuwa anamjua
mwanamke huyo katikati ya kesi hiyo, Karima el-Mahroug, anafahamika
vyema kwa jina lake la utani, Ruby the Heart Breaker, ametoa ushahidi.
Alikuwa ana umri wa miaka 17 wakati
huo anadaiwa kufanya kitendo hicho, lakini sasa amefikisha miaka 24.
wakati umri wa kufanya ngono Italia ni miaka 14, na ni kinyume cha
sheria kumlipa binti aliye chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya ngono.
El-Mahroug aliitwa kwa utetezi, lakini
akashindwa kutokea kwa sababu kadhaa,kuchelewesha hukumu. Timu ya
Berlusconi mara moja ikamengua katika orodha ya mashahidi. Chanzo: AFP
No comments:
Post a Comment