TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 17, 2013

KIONGOZI WA AL-QAIDA AFARIKI 
Kundi la wanamgambo la Al- Qaida katika kanda ya Islamic Maghreb limeripotiwa kuthibitisha kifo cha mmoja wa makamanda wake Abdelhamid Abou Zeid. Mkuu huyo aliuliwa katika mapigano na majeshi ya ufaransa kaskazini mwa mali mnamo mwezi wa machi.   
 
Shirika la habari la Mauritanian limesema limepokea taarifa kutoka kundi la wanamgambo likisema kuwa kiongozi wao Abou Zeid aliuwawa wakati akipigana na vikosi vya usalama vya ufaransa na chad kaskazini mwa mali.
 
Taarifa hiyo inasema wanachama wengine wa kundi linalopigana vita vya kidini waliuwawa wakati wa mapambano hayo akiwemo kiongozi mwingine wa la- qaida Al Chinghitty.
 
Chad na ufaransa zilitangaza kifo cha Abou zeid mwezi machi baada ya mapigano katika milima ya Ifoghas huko Mali lakini hakukuwa na uthibitisho rasmi kutoka kwenye kundi la al- qaida katika kanda ya Afrika Magharibi mpaka Jumapili.
 
Abou Zeid aliyezaliwa Algeria alijulikana kwa kuhusika kwake katika utekaji wa raia wa ulaya kwenye kanda ya Sahel ya Afrika. Alihusishwa na mauji ya mtalii wa kingereza mwaka 2009 Edwin Dyer na mfanyakazi wa msaada wa ufaransa Michel Germaneau mwaka uliofuata.
 
Fedha za malipo ya fidia kutokana na utekaji huo zilisaidia kufadhili Al- Qaida katika kanda hiyo Islamic Maghreb ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa wanamgambo wa kiislamu kuchukua udhibiti kaskazini mwa Mali.Chanzo:voaswahili

No comments:

Post a Comment