TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, June 16, 2013

BRAZIL YAINYUKA JAPAN 3-0 MABARA NEYMAL AANZA VEMA
brazil3 821f2brazil dad0c
Wachezaji wa Brazili wakishangilia mabao kwa wakati tofauti
MSHAMBULIAJI mpya wa Barcelona,Neymar jana aling'ara katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mabara, akifunga bao la mapema dakika ya tatu wakati Brazil inailaza 3-0 Japan.

Mshambuliaj huyo nyota wa Brazil, alifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari, akiunganisha pasi ya Fred ambaye naye alipokea krosi ya Marcelo kwa kifua kwanza.
Paulinho alifunga la pili dakika ya 48 kwa pasi ya Dani Alves na Jo akafunga la tatu dakika ya 90.
Ushindi huo unaiweka Brazil kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu. Italia na Mexico watamenyana leo katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Kikosi cha Brazil jana kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo, Paulinho, Fred/Jo dk81, Neymar/Lucas Moura dk74 na Hulk/Hernanes dk75.
Japan: Kawashima, Konno, Nagatomo, Uchida, Yoshida, Endo/Hosogai dk77, Honda/Inui dk88, Kiyotake/Maeda dk51,Kagawa, Hasebe na Okazaki.

No comments:

Post a Comment