TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 24, 2013

KONE AGOMBEWA NA LIVERPOOL 
kone 9deb0
Kone

kone2 48784
KOCHA wa Norwich, Chris Hughton anapambana kuipiga bao Everton katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Wigan, Arouna Kone
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast una thamani ya Pauni Milioni 5. Msimu uliopita amefunga mabao 13 na kuisaidia Wigan kutwaa Kombe la FA. Hull, Liverpool na Crystal Palace zote zinamtaka pia.
Jumapili, Kone alizipigia kengele klabu kubwa baada ya kusema hayuko tayari kucheza Daraja la Kwanza, kufuatia Wigan kushuka daraja.
Akizungumza na The Sun, nyota huyo wa zamani wa PSV Eindhoven alisema: "Wakati wote una malengo kama mchezaji, na siko tayari kucheza ligi ya pili England.
"Wigan imeshuka, ambayo ni aibu kubwa. Ni juu yao kuweka mambo sawa juu ya mipango yangu. Mimi ni wa kucheza moja ya klabu bora England,  na natumai nitapata nafasi. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment