TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, June 21, 2013

ARSENAL YAKUBALI KUMLIPA HIGUIN PAUND 150,000 KWA WIKI
arsenal 0c27e
Gonzalo Higuin
KLABU ya Arsenal imekubali kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki Gonzalo Higuain kuelekea usajili wa rekodi wa klabu hiyo wa Pauni Milioni 22.
Arsenal imekubali kutoa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 22 kwa Real Madrid kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Kiwango hicho kinavunja rekodi ya sasa ya klabu hiyo kununua mchezaji kwa bei kubwa, Pauni Milioni 15 ambazo ililipa kwa Zenit St Petersburg kumnunua Andrey Arshavin  Januari mwaka 2009. 

Nyota huyo wa Real Madrid ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu na Arsenal ipo karibu kabisa kumnasa mchezaji huyo ambaye imekuwa ikimmezea mate tangu akiwa River Plate, timu yake ya kwanza mwaka 2004.
  
Arsenal ilijaribu kutaka kumsajili mshambuliaji huyo Muargentina mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini ikazidiwa kete na Real Madrid.
Lakini Wenger sasa anakaribia kukata kiu yake ya kumsubiri kwa muda mrefu Higuain majira haya ya joto.

Arsenal pia imeendelea na nia yake kutaka kuwasajili Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la Higuain linaonekana kuwa la ukweli zaidi. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment