MISS REDD'S KANDA YA NYANDA ZA JUU KUPATIKANA LEO
Kinyang’anyiro
 cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kinatarajiwa kufanyika 
kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet uliopo Soweto Jijini 
Mbeya.   Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet, amesema baada ya 
warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa kambini tangu Juni 
25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja Juni 
29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana.   Ameongeza kuwa Shindano hilo
 limeandaliwa na Lake Victoria Arts & Culture Promotion chini ya 
Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha
        
                        
        
        
        
 REDDS, SBC kupitia  Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony
 Fm na Bomba Fm radio.   Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na 
burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na 
kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa  shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida 
na 25,000/= kwa VIP.   Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka 
kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania 
Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake  kuwa 
ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca 
Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1).  
 Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary
 Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4), 
Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2.   Kwa
 Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones  ambaye ndiye 
anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote 
wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi 
kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Picha na Mbeya yetu Blog
No comments:
Post a Comment