TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, June 19, 2013

NIGERIA YAWAFUNGA OCEANIA 6-1
nigeria 83dcb
Wachezaji wa Nigeria
nigeria2 2e5e1
 
nigeria3 49e37
TIMU ya taifa ya Nigeria imeifumua kwa mabao 6-1 Tahiti katika Kombe la Mabara usiku huu.
Jonathan Tehau aliifungia Tahiti, lakini Nnamdi Oduamadi akaifungia Super Eagles mabao matatu peke yake.
Mabingwa wa Oceania, Tahiti, wakiwa na mchezaji mmoja tu wa kulipwa kikosini, walikuwa wana mwanzo mgumu katika mchezo huo wa Kundi B wakati mpira ulipomgonga refa na kumkuta mchezaji wa Nigeria, Uwa Echiejile ambaye alifunga kwa shuti la kubabatiza dakika ya tano.
Nigeria ikapata bao la pili lililofungwa na Oduamadi dakika tano baadaye.
Tahiti iliwanua vitini mashabiki wake wakati Tehau alipofunga bao dakika ya 54.
Lakini Nigeria iliendelea kung'ara wakati Tehau alipojifunga kabla ya Oduamadi kukamilisha Hat-trick yake na Echiejile akafunga bao lake la pili kwenye mchezo huo.
 Enyeama, Ambrose, Omeruo, Oboabona, Echiejile, Ogude, Mikel, Mba, Oduamadi Ujah na Musa.
Tahiti: Samin, A Tehau, Vahirua, Lupion, Caroine, Bourebare, Vallar, Chong Hue, Aitamai, J Tehau na Simon. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment