BFT:UCHAGUZI UTAFANYIKA JULAI 7
Yah:- Uchaguzi wa viongozi wa BFT.
Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha
kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika ofisi za BFT
kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi
utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha
watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha kwa
kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria
mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba
yetu.
Upotoshaji
huo unafanywa na Akaroly Godfrey aliyekuwa kiongozi katika uongozi
uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya na
kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia
(AIBA) na kusababisha kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri zote
za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali
kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na
kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.
Fomu za
uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka
tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini
Mwanza na tarehe hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na
kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika
jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na
tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT
inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika uchaguzi
uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, waendelee na
shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa
kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013
BFT
inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza
wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.
No comments:
Post a Comment