SPURS YATAKA KUSAJILI MBRAZILI ANAYENG'ARA KOMBE LA MABARA
Paulinho anaweza kutua White Hart Lane
Leandro Damiao amekuwa akitakiwa kwa muda mrefu Tottenham
KLABU ya Tottenham inataka kukata
Pauni Milioni 15 kwa ajili ya kiungo Mbrazil, Paulinho kupambana na Roma
na Inter Milan ili kuinasa saini yake.
Mpango huo unakuja baada ya Fenerbahce kufufua nia ya kumnunua mshambuliaji Emmanuel Adebayor ambaye atawasaidia kupata fedha.
Paulinho, mwenye umri wa miaka 24,
ambaye jina lake kamili ni Jose Paulo Bezerra Maciel Junior, alitarajiwa
kusaini kwa moja ya timu za Italia wiki hii baada ya kufikia
makubaliano ya awali.
Pamoja na hayo, nyota huyo wa Corinthians inaelezwa anapenda kuhamia Ligi Kuu ya England.
Tottenham inaweza kutakiwa kupanda dau
kidogo hadi Pauni milioni 18 pamoja na kwamba wanahamasika na kujua
mchezaji huyo anapenda kuhamia London.
Akizungumza nchini Brazil, Naibu
Mkurugenzi wa Corinthians, Duilio Monteiro Alves, alisema: "(Tottenham)
ni klabu ambayo tunafahamu ina nia, lakini bado hakuna kitu rasmi
kilichofanyika. Dhahiri itakuja. Tunatarajia siku zijazo.
"Lengo letu ni kumzuia, lakini acha tusubiri na tuone; ikiwa ni nzuri kwake, nzuri kwa Corinthians, tutafanya uamuzi,".
Kiungo
wa Atletico, Mineiro Bernard, mwenye umri wa miaka 20, pia anatakiwa na
mshambuliaji wa Internacional, Leandro Damiao anabaki kuwa suluhisho
wakati Mbrazil mwingine, beki kinda wa miaka 18 wa Botafogo, Doria,
amekuwa akijadiliwa.
Paulinho amezivutia Roma, Inter na Tottenham, lakini amesema hatatoa uamuzi hadi baada ya Kombe la Mabara.
Kuwasili kwake White Hart Lane
kutafungua milango ya watu kuondoka Spurs, kama inavyofahamika Fulham
inamtaka Tom Huddlestone na mkongwe mwenye umri wa miaka 32, Scott
Parker, ambaye anatakiwa Sunderland. Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment