CHELSEA YAFIKA BEI KWA CAVANNI,YALIPA PAUNI 49 KWA NAPOLI

Mshambuliaji wa Uruguay na Napoli, Edinson Cavanni

KITUO cha Redio cha Napoli, Marte 
kimetangaza kwamba dau la Pauni Milioni 49.3 limetolewa na Chelsea kwa 
ajili ya mshambuliaji  Edinson Cavani ambaye muda wote anampasua kichwa 
mmiliki wa klabu ya Chelsea Bilionea Roman Abramovich mwenye lengo la 
kuimarisha kikosi chake chini ya kocha Jose Mourinho.
Katika taarifa ya jana usiku, Radio 
Marte ilitangaza: “Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya 
kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.
“Rafa Benitez pia amebariki, lakini 
kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba
 pengo la Il Matador.
“Aurelio De Laurentiis”, klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
“Mchezaji huyo atajiingizia mshahara 
wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,”. Habari zimevuja
 kama kwamba Cavani ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, 
Aurelio de Laurentiis na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo 
kwenye mbio hizo. 
Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba 
yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya 
Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa 
iliyotolewa na Chelsea. Chanzo: Baraka Mpenja
No comments:
Post a Comment