SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU ( MOSES MACHALI) AKIWA DODOMA JANA JIONI
 Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana jioni mjini Dodoma.
Tukio hilo lilitokea jana jioni  wakati Mh. Machalli 
akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya 
kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara 
ili wasogee pembeni naye aweze kupita ....
Kitendo hicho  kilionekana 
kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa 
nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli 
kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni ....
Baada ya kushuka,  vijana 
hao walimtolea  matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa 
hasira ndipo kipigo kikali kilipoanza. 
Shuhuda aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Shuhuda aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.
No comments:
Post a Comment