TENDWA AKIPA USAJILI WA KUDUMU CHAMA KIPYA CHA 21

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa (kulia) akizungumza na wana CHAUMMA

Tendwa akikabidhi cheti cha usajili CHAUMMA

Baadhi ya wanachama cha CHAUMMA pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kupewa usajili
Na Thehabari.com
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, 
John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama cha Ukombozi wa Umma 
(CHAUMMA) huku akivitaka vyama vya siasa kufuata sheria na kuepuka kuwa 
vyanzo vya vurugu na uchochezi wa migogoro.
Tendwa ameyasema hayo leo jijini Dar 
es Salaam alipokuwa akiwakabidhi cheti cha usajili wa kudumu viongozi wa
 chama kimpya cha kinachojulikana kama Chama cha Ukombozi wa Umma.
Alivitaka vyama vya siasa kuhakikisha 
vinatimiza malengo yao ya kushika dola na hata kama itashindikana kwao, 
basi kuhakikisha wanapata nafasi za uwakilishi wa wananchi zikiwemo za 
udiwani, ubunge pamoja na uongozi wa serikali za mitaa kwa mujibu wa 
taratibu za nafasi hizo.
Alisema kwa sasa vipo vyama vya siasa 
ambavyo licha ya kuwa na usajili wa kudumu na uongozi mzuri usio na 
migogoro vimeshindwa kutimiza malengo ya msingi ya chama kwa kushika 
nafasi za uwakilishi maeneo anuai kwa mujibu wa utaratibu.
"...Vyama hivi unakuta hawana mbunge, 
hawana diwani, hawana viongozi serikali za mitaa, kijiji na kwingineko 
lakini ukiangalia wana viongozi wazuri hawana migogoro ndani ya chama, 
haya sio madhumuni ya chama cha siasa," alisema Tendwa.
Aidha aliwataka viongozi wa CHAUMMA 
kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze kutimiza malengo ya chama na 
kuwawakilisha wananchi maeneo mbalimbali ya uongozi kisiasa. Alisema 
katika mapendekezo mapya ofisi yake inafikiria kuanza kuvipunguza vyama 
ambavyo licha ya kuwa na usajili havifanyi chochote kama ilivyo kwa 
madhumuni ya kuanzisha chama.
"Sheria inafanyiwa marekebisho, chama 
kikikaa ndani ya miaka mitano hakijafanya chochote tunafikiria kukifuta,
 kiongozi wa chama akitukana miezi sita unafungiwa kwa muda...maana 
hatuwezi kuruhusu matusi, vurungu na masuala mengine yasiokuwa na msingi
 ndani ya vyama vya siasa," alisema Tendwa.
Hata hivyo amesema katika mapendekezo 
yao ya mabadiliko ya katiba wamependekeza mambo mengi ikiwemo sasa 
kuruhusu vyama kujiunga na kufanya shughuli za siasa kama ilivyo kwa 
nchi za Kenya, Afrika Kusini, Lethoto na nchini Namibia.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa 
cheti cha usajili wa kudumu Mwenyekiti wa muda wa CHAUMMA, Wallance 
Mayunga alisema wamejipanga vizuri katika kuwatumikia wananchi na chama 
chake kinatambua changamoto zilizopo nchini katika uongozi, utendaji na 
utawala hivyo kina nia ya kuleta mabadiliko.
Nafasi ya Katibu Mkuu wa muda wa 
CHAUMMA inashikiliwa na Shaffii Abed huku Hamad Tao akiwa ni miongoni 
mwa wanachama waanzilishi wa nchama hicho.
~Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:
Post a Comment