HISPANIA YATWAA UBINGWA U21 YAIBAMIZA ITALIA 4-2
Hispania U-21 wakishangilia ubingwa baada ya kuibamiza Italia 4-2
Hispania wakishangilia
Thiago Alcantara amefunga mabao matatu kipindi cha kwanza kuipa ushindi Hispania
KIUNGO Thiago Alcantara amekuwa
kivutio katika ushindi wa kikosi cha vijana cha Hispania chini ya miaka
21 wa mabao 4-2 dhidi ya Italia na kutwaa Kombe la Ulaya kwa vijana
barani humo, baada ya mchezaji huyo anayetakiwa na Manchester United
kufunga mabao matatu mjini Jerusalem.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wa Barcelona amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Old Trafford.
Alcantara, aliyekuwamo kwenye kikosi
cha Hispania kilichoshinda taji hilo miaka miwili iliyopita nchini
Denmark, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya sita, lakini
Italia ikasawazisha haraka kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 10.
Thiago akafunga tena dakika ya 31 na
38 kwa penalti, kabla ya Isco kufunga dakika ya 66 kwa penalti pia na
Borini akaifungia Italia dakika ya 79 kufanya 4-2.
Kikosi cha Hispania leo kilikuwa; De
Gea, Montoya, Bartra, Martinez, Moreno, Koke/Camacho dk86, Illarramendi,
Thiago, Tello/Muniain dk70, Morata/Rodrigo dk80 na Isco.
Italy U21; Bardi, Donati, Bianchetti,
Caldirola, Regini, Florenzi/Saponara dk58, Rossi, Verratti/Crimi dk76,
Insigne, Borini na Immobile/Gabbiadini dk58. Chanzo: sportmail
No comments:
Post a Comment