WALIMU KENYA WAANZA MGOMO
Walimu wa
shule za sekondari na taasisi za juu nchini Kenya wameanza rasmi mgomo
wao wa kitaifa hii leo baada ya kukosa kuafikia mwafaka na serikali
kuhusu kutengewa pesa za kuwalipa marupurupu.
Mgomo huu unakuja baada ya kusomwa kwa
bajeti ya serikali wiki jana. Walimu hao wanalalamika kuwa serikali
imetenga mabilioni ya pesa kwa ununuzi wa vipakatilishi kwa wanafunzi wa
darasa la kwanza badala ya kutumia pesa kwa miradi mingine ambayo ni
muhimu zaidi katika sekta ya elimu.
Walimu hao wanasema wataendelea na mgomo wao hadi serikali itakapokubali kuwatimizia matakwa yao.
Pamoja na hilo chama cha walimu hao,
kimewataka wanchama wake kusalia nyumbani na kutofunza na badala yake
kufika katika makao makuu ya chama cha walimu kwa maagizo zaidi kuhusu
hatua wakatazochukua.
Walimu hao wanataka wapewe marupuru ya
safari zao pamoja na majukumu ya usimamizi wa shule kuwa sawa na yale
wanayolipwa wafanyakazi wengine wa umma.
Pia wanataka swala la kupandishwa vyeo kupewa kipaombele. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment