TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, June 24, 2013

BAYERN WAMTAMBULISHA RASMI PER GUARDIOLA
pep 59b80
Kocha mpya wa Bayern, Pep Guardiola akizungumza mara baada ya kutambulishwa rasmi

pep2 d5981
Watu walihudhuria kutambulishwa kwa Pep
pep3 324e7
  
pep4 e4433
WASHINDI wa mataji matatu, Bayern Munich wamemtambulisha kocha wao mpya, Pep Guardiola leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, The Bavarians wakijiandaa kuendelea kutamba katika soka ya nyumbani na Ulaya.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amesema yuko tayari kukabiliana na changamoto za kufundisha timu iliyofanya vizuri msimu uliopita chini ya Jupp Heynckes, ikishinda mataji ya Ligi Kuu ya nyumbani na makombe mawili, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Lazima nikubali mlinganisho" alisema Guardiola, akiwa katika vazi nadhifu la suti ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu akizungumza Kijerumani kwenye Mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa klabu, Allianz Arena.
"Lazima niwe tayari kuishi na hiyo. Nipo chini ya shinikizo, wazi, lakini nafahamu hili na nakubali changamoto hii bila woga na ndiyo maana mimi ni kocha,"alisema.
Guardiola, ambaye aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne ya kuwa na Barcelona, usajili wake ni mkubwa Bayern na hasa ikizingatiwa anahamia timu iliyofanya vyema. Alitumia mwaka wake mzima baada ya kuacha kazi Hispania mwaka 2012, kwa kupumzika New York, Marekani.

"Kitu nachofikiria kwa sasa ni zawadi, baraka kuwa hapa na Bayern,"alisema kocha huyo Mspanyola, aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment