MTANZANIA ATEULIWA KULIONGOZA JESHI LA KULINDA AMANI HUKO DARFUR
Lt.
 Jenerali  Paul Ignace Mella,Mkuu Mpya wa Jeshi la Mseto kati ya   Umoja
 wa Mataifa na Umoja wa Afrika maarufu kama UNAMID linalolinda Amani 
huko   DARFUR  Nchini Sudan. 
Lt. Jenerali. Mella kutoka  Jeshi la 
Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) anachukua nafasi iliyoachwa na  Lt. 
Jenerali Patrick Nyamvumba kutoka  Rwanda ambaye amemaliza muda wake 
Machi 31,2013. 
---------
Kwa mara nyingine  Bendera ya  Tanzania imeendelea kupepea katika Tasnia ya Ulinzi wa Amani ya Kimataifa. 
Mapema
 wiki hii,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na Mwenyekiti 
wa Umoja wa Afrika Bi. Nkosizana Dlamin Zuma wametangaza uteuzi wa 
Luteni General Paul Ignace Mella  Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (
 JWTZ) kuwa Mkuu  Mpya wa Jeshi la   Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa 
huko Darfur ( UNAMID) 
Taarifa
 iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki Moon, 
na nakala yake kutumwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  imeeleza kwamba,  Lt. 
Gen. Mella anachukua  nafasi iliyoachwa na Mkuu wa  zamani wa Jeshi hilo
 (UNAMID), Lt. Gen Patrick Nyamvumba kutoka Rwanda ambaye amemaliza muda
 wake wa  utumishi  March 31,2013. 
Wasifu
 wa Luteni General Paul Ignace Mella unaelezwa  kuwa ni Mwanajeshi wa 
muda mrefu na  mwenye uzoefu na utumishi uliotukuka katika JWTZ akiwa 
amewahi kushika nyadhifa  mbali mbali  muhimu za uongozi. 
Baadhi
 ya nyadhifa hizo ni pamoja na Naibu Kamanda Kikosi cha Tanzania chini 
ya Umoja wa Mataifa huko Liberia (  1993-95), Kamanda wa Kikosi cha  
JWTZ, Afisa Mnadhimu-Makao Makuu  ya Jeshi, Mwambata Jeshi-Ubalozi wa 
Tanzania Uganda na hadi sasa alikuwa ni Mkuu wa Usalama na Utambuzi- 
JWTZ. 
Uteuzi
 wa Lt. Generali Mella unafuatia mchakato mrefu ulioshindanisha 
wateuliwa kutoka nchi mbalimbali duniani, na hatimaye  yeyé akaibuka 
mshindi.

No comments:
Post a Comment