TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, June 21, 2013

LIVERPOOL YAMSAJILI LUIS ALBERTO KUZIBA PENGO LA SUALEZ
liver2 45be1Luis Suarez

liver cbdfb
Luis Alberto
MSHAMBULIAJI wa Sevilla, Luis Alberto atafanyiwa vipimo vya afya Liverpool kesho baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kuuziana nyota huyo kwa Pauni Milioni 6.8.

Kinda huyo wa umri wa miaka 20, ambaye atasaini Mkataba wa miaka minne, amekuwa akicheza kwa mkopo Barcelona B na alitarajiwa kubaki Sevilla, lakini kwa fedha iliyotolewa klabu hiyo imeamua kumuacha aondoke.

Barcelona imeamua kuachana na nia ya kumsajili moja kwa moja baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo, na Alberto atakuwa mshambuliaji wa pili kusajiliwa Liverpool baada ya Iago Aspas kutoka Celta Vigo

Usajili huu unaleta shaka juu ya mustakabali wa mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez, ambaye amekuwa akihusishwa na kuondoka majira haya ya joto.

Habari hizo zinakuja siku moja baada ya Mkurugenzi wa Michezo wa Sevilla, Monchi kusema ofa iliyotolewa na Liverpool ni kiduchu kwa Alberto - lakini klabu hiyo ya Merseysiders imekamilisha mpango.
Alberto ameichezea mara moja timu ya taifa ya vijana ya Hispania chini ya umri wa miaka 21, na amefunga mabao 11 katika mechi 38 alizoichezeaBarcelona B. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment