TAIFA STARS KAMBINI TENA JULAI 4
Kocha wa
Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka
huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika
kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika
Kusini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada
ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya
Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kim amesema wachezaji watakaoitwa
kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi
Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe,
Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank
Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon
Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni
Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala. Chanzo: Boniface Wambura

No comments:
Post a Comment