CATHY WA BONGO MOVIE ALIA NA USHIRIKINA ULIPO NDANI YA TASNIA HIYO....AWATAKA WASANII WAMRUDIE MUNGU
Mwigizaji wa Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’  naye amenyanyua kinywa chake na 
kuonesha jinsi gani anakerwa na wasanii wanaoshinda kwa waganga ili 
kutafuta ustaa.
Akiongea na mwandishi  wetu hivi karibuni, Cathy alisema kuna baadhi 
ya wasanii (hakuwataja majina) wamekuwa na tabia za kuzunguka kwa 
waganga wakitafuta kuwa juu katika tasnia ya filamu suala ambalo 
halipendezi na kuwasihi wawe na hofu ya Mungu.
“Vifo vya wasanii 
vimetokea vingi sana, nilidhani kutokana na vifo hivyo wangepata hofu ya
 Mungu na kuacha mambo yasiyofaa vikiwemo vitendo vya kishirikina lakini
 hawakomi, wananikera sana. Ipo siku wataumbuka kwani Mungu siyo 
binadamu,” alisema Cathy.

No comments:
Post a Comment