MURINHO ATAKA WATANO KUIMARISHA CHELSEA 
KOCHA Jose Mourinho amewalenga wachezaji watano kuwasajili baada ya kurejea Chelsea kwa mara ya pili.
Wachezaji wa mwanzoni anaowataka 
wanafahamika ni washambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic, Manchester 
City, Edin Dzeko, sentahafu wa Porto, Eliaquim Mangala, Daniele De Rossi
 wa Roma na kiungo Mbrazil, Fernandinho wa Shakhtar Donetsk.
Mourinho pia ameweka wazi kumrejesha 
to Romelu Lukaku, baada ya kufanya vizuri msimu huu akiwa na West Brom 
ambako amefunga mabao 17, kwamba hataki atolewe kwa mkopo tena.
Kevin de Bruyne, ambaye ameomba kuuzwa
 moja kwa moja Borussia Dortmund baada ya kucheza kwa mkopo Werder 
Bremen, atakutana na kocha huyo mpya kabla ya kufikiwa uamuzi juu ya 
mustakabali wake.
Lakini Mourinho amesistiza hatafanya mabadiliko makubwa msimu huu.



No comments:
Post a Comment