AZIMIO LA KUPAMBANA NA MANYANYASO YA NGONO
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limeidhinisha kwa kauli moja azmio la kuimarisha njia za kupambana na
manyanyaso ya ngono yanayotumiwa kama silaha ya kivita.
Taasisi za Umoja wa Mataifa zinakisia kuwa zaidi ya wanawake elfu 40 walibakwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia kati ya mwaka wa 1989-2003 na katika iliyokuwa Yugoslavia zamani, wanawake elfu 60 walibakwa mapema miaka ya 1990 na wengine laki mbili katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tangu mwaka wa 1998.
Syria sasa imeongezewa kwenye orodha hiyo, huku kukiw ana ripoti za wanawake na wasichana na hata wavulana waliobakwa kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea.
Umoja wa Mataifa unasema hiyo ni mifano michache tu na kwamba hata baada ya kumalizika kwa mitafaruku manyanyaso ya ngono huendelea ambapo wasichana na wanawake wanatunga mimba au kuambukizwa magonjwa ya zinaa , kutengwa na jamii na hata kubaguliwa.
Azmio la Jumatatu la baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalenga kuimarisha njia zote katika mfumo wa Umoja wa Mataifa kupambana na ubakaji wakati wa vita ikiwa ni pamoja na kuwapeleka washauri wa kijinsia,walinda amani na tume za kisiasa katika maeneo yaliyoathiriwa na hata kuweka vikwazo kwa wanaofanya manyanyaso ya kingono.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague alisema manyanyaso ya ngono kama silaha ya kivita ni sawa na bunduki na vifaru, ambavyo vinalenga kutenganisha na kuvuruga jamii ili kufikia malengo ya kijeshi na lazima hilo lifike kikomo.
Mcheza filamu mashuhuri wa Marekani Angelina Jolie ambaye pia ni balozi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa maswala ya wakimbizi alihutubia kikao hicho cha Jumatatu. Chanzo: voaswahili

No comments:
Post a Comment