ETHIOPAI, MISRI KUZUNGUMZA ZAIDI JUU YA MTO NILE
Ujenzi wa bwawa la kufua umeme, nchini Ethiopia
Ethiopia
na Misri wamekubaliana kufanya mazungumzo ya ziada juu ya athari za
bwawa kubwa ambalo Ethiopia inalijenga kwenye mto Nile.
Wiki iliyopita Rais wa Misri, Mohammed
Morsi alisema hataki vita lakini ataweka mapendekezo yote wazi
yanayohusu majibu ya nchi yake kwa mradi wa bwawa hilo ambalo Misri
inawasi wasi utapunguza sana kiwango cha usambasaji wake wa maji.
Maafisa wa Ethiopia walijibu wakisema
hawatasitisha ujenzi wa bwawa la Grand Ethiopian Renaissance Dam wenye
gharama ya takribani dola bilioni 5.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Mohamed Kamel Amr alisema Jumanne kwamba taarifa zilizotolewa awali zilitokana na “jazba za wakati huo”.
Amr alikutana na kiongozi mwenzake wa Ethiopia, Tedros Adhanom, siku ya Jumatatu na Jumanne katika mji mkuu wa Ethiopia. Wote walisema wataendelea na mazungumzo kuhusu bwawa la usambazaji umeme ikiwemo mazungumzo zaidi ya kiufundi.
No comments:
Post a Comment