BRAZIL YAIBAMIZA MEXICO 2-0
Neyman akishangilia baada ya kufunga bao
Wachezaji wa Brazil wakishangilia
Nayman akimtoka beki wa Mexico
Shabiki wa Brazil
TIMU ya taifa ya Brazil imeshinda
mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara, huku kijana mdogo mwenye kipaji
cha ajabu, Neymar akifunga bao tamu ndani ya dakika 10 za kwanza kabla
ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Jo.
Brazil imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
Daniel Alves alipinda krosi kutoka
kulia na nyota mpya wa Barcelona, Neymar akaitokea wa kwanza mbele ya
beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya
tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na
refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves,
Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62,
Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred.
Mexico: Corona, Rodriguez, Salcido,
Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno, Guardado, Torres/Barrera dk70,
Mier na Flores/Herrera dk68.
No comments:
Post a Comment