ABIDAL AAGWA BARCELONA
Abidal
Abidal akimwaga machozi wakati akiaga
BEKI Eric Abidal jana alihitimisha miaka yake sita Barcelona na kufanyiwa tafrija nzuri ya kuagwa ndani ya Uwanja wa Nou Camp.
Beki huyo Mfaransa mwenye umri wa
miaka 33, ambaye alirejea uwanjani baada ya kupona matatizo ya ini,
alipewa jezi ya fremu ya Barca iliyoandikwa 'Merci Abi' na akanyanyuliwa
juu na wachezaji wenzake.
Cesc Fabregas, anayetakiwa na
Manchester United, Manchester City na Arsenal, na David Villa,
anayetakiwa na The Gunners na Tottenham, wanaweza kuwa walicheza mechi
yao ya mwisho katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Malaga.
Abidal aliingia uwanjani akitokea
benchi dakika ya 75 kuwaaga mashabiki baada ya kutangaza hatasaini tena
msimu mwingine mapema wiki hii huku akibubujikwa na machozi.
Abidal alisajiliwa kama mchezaji huru
kutoka Lyon mwaka 2007 na amecheza karibu mechi 200. Katika miaka yake
sita ameshinda mataji manne ya La Liga, mawili ya Ligi ya Mabingwa,
mawili Kombe la Mfalme, matatu ya Super Cup ya Hispania na mawili ya
Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
Pia aliingizwa kwenye timu ya UEFA ya mwaka 2007 na akashinda tuzo ya beki bora La Liga mwaka 2011.
Kimataifa alikuwemo kwenye kikosi cha
Ufaransa kilichoshika nafasi ya pili katika Kombe la Dunia mwaka 2006 na
amecheza jumla ya mechi 61 katika timu hiyo. Pia ameshinda mataji
matatu ya Ligue 1 akiwa na Lyon.
Katika Mkutano na Waandishi wa Habari
mapema wiki hii alisema: "Ningependa kubaki, lakini lazima nikubaliane
na uamuzi wa klabu (kutoniongezea mkataba).
"Nimecheza hapa kwa miaka sita, na
umekuwa uzoefu mkubwa katika maisha yangu. na nilikuwa nina malengo
mawili: kupambana mabinti zangu wakue na kucheza tena.
"Nataka kuwashukuru mashabiki wote wa klabu ambao walinisapoti.
"Timu ni familia yangu ya pili. Tumepitia mengi pamoja na nitakumbuka hii daima. NakwendaI, nitahakikisha narudi,"alisema.
Fabregas na Villa wote wanaandamwa na
tetesi za kuondoka kwenda kucheza Ligi Kuu England na kiungo wa zamani
wa Arsenal, anatarajiwa kuwa na mazungumzo na kocha Tito Vilanova wiki
ijayo. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment