WAZIRI WA MISRI ANUSURIKA SHAMBULIZI LA BOMU
Waziri wa mambo ya ndani wa Misri
Mohamed Ibrahim amenusurika kutokana na jaribio la kutaka kumua
lililosababisha takriban watu saba kujeruhiwa. Maafisa wa usalama wa
Misri wanasema bomu lililengwa kushambulia msafara wa magari ya waziri
Ibrahim karibu na kiunga cha Nasr City kaskazini mashariki ya Cairo.(P.T)
Ibrahim alisema hakujeruhiwa katika
mlipuko huo uliotokea karibu na nyumbani kwake. Alisema mwanzoni mwa
wiki hii kwamba aliarifiwa mipango ya kutaka kuuwawa na kwamba watu wa
nje walihusika. Mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Fattah al-sisi alimpatia
gari maalumu la ulinzi.
Waziri Ibrahim alihusika katika kusimamia msako wa kutumia nguvu dhidi ya wafuasi wa Rais Mohamed Morsi, kiongozi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia kutoka chama cha ki-islam na kuondolewa madarakani miezi miwili iliyopita na jeshi la Misri kufuatia maandamano makubwa ya raia dhidi ya utawala wake.
Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika kwa shambulizi hilo ambalo ni linasemekana ni mlipuko mkubwa kabisa wa bomu tangu serikali ya mpito kuchukua madaraka.
Chama cha Muslim Brotherhood cha bwana Morsi kinachoshutumiwa na serikali kwa ugaidi na kuchochea ghasia kimelaani kitendo cha alhamis. Lakini kimefafanua juu ya hatari ambazo ghasia za kisiasa Misri zitaweza kuchochea wimbi la mashambulizi ya wanaharakati wa ki-islam kama yale yaliyotokea miaka ya 1980 na 1990.

No comments:
Post a Comment