URUSI YASEMA AMANI YAWEZEKANA SYRIA
Sergei Lavrov na John Kerry wanakutana
Geneva Uswisi kujadiliana kwa kina kuhusu mpango uliopendekezwa na
Urusi katika kuzishughulikia silaha za sumu za utawala wa Assad
Urusi inapendekeza mpango wa hatua nne kwa marekani kutekeleza azma yake ya kutaka kuziharibu silaha za sumu za Syria.Taarifa hizo zimechapishwa na gazeti moja la mjini Moscow katika wakati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anatazamiwa kukutana leo na mwenzake wa Marekani John Kerry mjini Geneva.Suala hilo litajadiliwa kwa kina katika mkutano huo.(P.T)
Urusi inapendekeza mpango wa hatua nne kwa marekani kutekeleza azma yake ya kutaka kuziharibu silaha za sumu za Syria.Taarifa hizo zimechapishwa na gazeti moja la mjini Moscow katika wakati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anatazamiwa kukutana leo na mwenzake wa Marekani John Kerry mjini Geneva.Suala hilo litajadiliwa kwa kina katika mkutano huo.(P.T)
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei
Lavrov amenukuliwa akisema bado kuna nafasi ya kupatikana amani nchini
Syria na ulimwengu haupaswi kuiacha nafasi hiyo ipite bila
kuitumia.Lavrov ametowa kauli hiyo mbele ya wanafunzi huko Kazakhstan
kabla ya kuelekea mjini Geneva baadae kwa ajili ya mazungumzo na
mwenzake wa Marekani John Kerry kuhusu pendekezo la nchi yake ambalo
limemfanya hata rais Obama kulitaka Bunge la nchi yake kuakhirisha zoezi
la kura ya kutowa ridhaa ya kushambuliwa Syria.
Lavrov ameridhsishwa na hatua ya Syria
ya kuridhia mpango wake wa kuitaka nchi hiyo izisabilie silaha zake za
sumu chini ya uangalizi wa Kimataifa.Aidha ameonya kuhusu kuchukuliwa
hatua za kijeshi dhidi ya Syria akisema ni jambo litakalozidisha mafuta
katika moto ambao tayari unawaka na kulitekeleza eneo zima.
Pingamizi la waasi
Hata hivyo kutoka Syria kwenyewe waasi
wamelipinga pendekezo la Urusi kuhusu kuzisalimisha silaha za sumu za
utawala wa Assad wakisema utawala huo unabidi kufikishwa mbele ya
mahakama ya Kimataifa kuhusiana na shambulio la mwezi uliopita
lililofanywa karibu na mji wa Damascus ambako silaha za sumu zilitumika
na mamia ya watu waliuwawa.
Jenerali Salim Idrsi ambaye ni kamanda
wa ngazi ya juu wa jeshi la waasi nchini humo amesema silaha za sumu
zilikuwa chombo cha uhalifu katika shambulio hilo la Agosti 21 katika
mji wa Ghouta.Tamko hilo la waasi linakuja saa chache kabla Kerry
kuwasili Geneva kwa ajili mkutano wake na Lavrov.Pamoja na hayo Waziri
wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Lareunt Fabius amebaini kwamba ripoti ya
wachunguzi wa Umoja wa Mataifa katika suala la kutumiwa silaha za sumu
nchini Syria huenda ikatolewa siku ya Jumatatu.
Akizungumza na redio moja ya kifaransa
waziri huyo ameweka wazi kwamba ripoti hiyo itaeleza kwamba yamefanyika
mauaji ya halaiki kwa kutumika silaha za sumu na kwamba ripoti hiyo
itabaini chanzo cha shambulio hilo.Wachunguzi hao waliondoka Syria
Agosti 31 baada ya kukusanya sampuli za ushahidi utakaowasaidia katika
uchunguzi wao kuhusu shambulio la Ghouta.
Msimamo wa Marekani
Marekani na washirika wake ambao ni
pamoja na Ufaransa wanasema ni utawala wa rais Bashar al Assad uliofanya
shambulio hilo lakini serikali hiyo ya mjini Damascus na mshirika wake
Urussi wanalitwika mzigo jeshi la waasi.Wajumbe kutoka nchi tano
wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
walikuwa na kikao katika Umoja wa Mataifa juu ya Syria ambacho
hakikufikia mwafaka hapo jana.
Mazungumzo ya Geneva kwahivyo
yanategemewa kuchukuwa siku mbili au tatu na pia yatajadili juu ya
kuzitia msukumo juhudi za kuitishwa mkutano wa amani unaonuiwa kumaliza
vita vya Syria.Lavrov na Kerry watakutana pia na Lakhdar Brahimi mjumbe
wa Kimataifa kujadiliana kuhusu mapngo wa kuwakutanisha waasi na utawala
wa Assad katika meza ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment