UN YAKOSOA TZ KWA KUWAFUKUZA WAHAMIAJI HARAMU
Umoja wa
Mataifa umesema kuwa takriban wahamiaji haramu elfu 25 kutoka Burundi
wameondoshwa Tanzania kwa nguvu katika mwezi mmoja uliopita.
Afisa wa
shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR amesema
malori yanayowasafirisha warundi yamekuwa yakivuka mpaka kila siku ,
huku wahamiaji haramu wengi wakikosa mahitaji muhimu kama vile maji na
chakula
hdg
Taarifa zinazohusianaTanzania
Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani .
Takriban
watu milioni moja walitoroka kutoka Burundi na kuingia Tanzania wakati
wa mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wakati vita vilipozuka mwaka 1993.
Wengi walirejea kwa hiari wakati amani ilipopatikana mwaka 2006.
Nchi hiyo
imekuwa makao kwa mamilioni ya wakimbizi katika kipindi cha zaidi ya
miaka kumi iliyopita kutokana na migogoro katika eneo la maziwa makuu.
Maafisa
wa Tanzania sasa wameanza kutekeleza amri ya kuwaondoa kwa nguvu wale
wanaodaiwa kuwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda, na Jamuhuri ya
kidemokrasia ya Congo.
Shughuli
hii imetokea wakati mmoja na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na
Rwanda ambayo imekuwa ikikanusha madai ya kuchochea vurugu katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mgogoro
ndani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nao unaendelea kuchochea idadi
ya wakimbizi wanaotoroka vita na kuingia katika nchi jirani.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment