TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, June 1, 2013

REAL MADRID YATOA PAUNDI MILLION 40 KUMNASA SUARES
suarez 94278
MSHAMBULIAJI Luis Suarez inaonekana yuko njiani kuondoka Anfield baada ya jana usiku, kuibuka madai kwamba Real Madrid imetoa ofa ya Pauni Milioni 40 kumhamishia Bernabeu.

Kiasi cha saa 24 baada ya mpachika mabao huyo wa Liverpool kuiambia Redio ya Uruguay itamuwia vigumu kuwakatalia Madrid wakimtaka, gazeti maarufu Hispania, Marca limeripoti kwamba makubaliano yamefikiwa kumfanya awe mchezaji wa Real.
 Liverpool wamekasirishwa na habari za kwamba Real imeanza mchakato wa kumsajili Suarez bila kuwasiliana na klabu ya mchezaji huyo. Imesema Suarez atakuwa amekiuka mkataba wake kufanya mazungumzo na Real bila ridhaa ya klabu.
 Suarez pia amewaruka Marca juu ya taarifa yao, ingawa bado mustakabali wake Anfield uko shakani. "Si kweli nina makubaliano na Real Madrid. Nafikiria mustakabali wangu, lakini bado sijaamua chochote,"alisema’
 Rais wa Real, Florentino Perez amemzungumzia mchezaji huyo na kusema: "Suarez ni mchezaji mkubwa, na nina uhakika klabu zote duniani zinamtaka. Nampenda,". Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment