MAELFU WAANDAMANA ADDIS ABABA KUTAKA WANAHARAKATI,WANAHABARI WATOLEWE KIZUIZINI
ya
waandamanaji wameandamana katika barabara za mjini Addis Ababa,
Ethiopia, wakidai waandishi wa habari na wanaharakati walioko kizuizini
wafunguliwe.
Waandishi wa habari wanasema ni nadra
kuonesha upinzani wa namna hiyo kwa chama tawala ambacho kinadhibiti
shughuli za jamii sawasawa.
Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu
yanasema serikali imetumia sheria za kupambana na ugaidi ili kuwafunga
waandishi wa habari.
Waandamanaji- wengi kutoka upinzani - walipiga kelele kudai uhuru na haki.
Haya ni maandamano ya kwanza tangu mwaka wa 2005 ambapo mamia ya waandamanaji waliuliwa katika ghasia zilizofuatia uchaguzi. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment