MAAFA YA ZANZIBAR
IKIWA
ni siku tatu tangu tukio la vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa
baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa tangi la maji, Chake Chake
mjini hapa, Uwazi lina simulizi ya namna tukio zima lilivyokuwa.Tukio hilo la kusikitisha lililokatisha ndoto za Watanzania wenzetu hao, lilitokea juzi, Jumapili mishale ya saa 3 asubuhi, Machomanne - Chake Chake, Pemba.
WALIOFARIKI
Hadi juzi Jumapili, ilifahamika kuwa waliofariki katika ajali hiyo ni watatu ambao ni Juma Rashid Juma (35) mkazi wa Chanjaani, Suleiman Mohammed Abdiadi ‘Golo’ (55) mkazi wa Kwale na Salum Muhidini Vuai ‘Bandudu’ (35) mkazi Madungu, wote wakiwa ni wenyeji wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Suleiman Hassan Suleiman, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema marehemu hao walifikwa na mauti wakiwa katika kazi ya kuteremsha ukuta wa mnara wa tangi la maji ambao walikuwa wameshaukata.

ILIKUWAJE?
Akielezea tukio lilivyokuwa, Kamanda Suleiman alisema, ukuta huo ulikuwa tayari umeshaweka ufa hivyo wakati wakiwa kazini kuuteremsha ndipo ulianguka na kuwaelemea marehemu hao pamoja na majeruhi waliokuwa juu wakiuteremsha.
Alisema, idadi ya mafundi waliokuwepo kazini hapo ni 12 ambapo watatu walipoteza maisha papo hapo na watatu kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Chake Chake huku wengine sita wakikimbia.

MAJERUHI WANATIA HURUMA
Hali za majeruhi watatu ambao ni Jackson John (26) mkazi wa Msingini, Ali Saleh Ali (35) mkazi wa Michakaeni na Yohana Richard (25) mkazi wa Machomanne zinaendelea vizuri.
Juma Ahmed, mkazi wa Chake Chake ambaye alifika hospitalini hapo kuwajulia hali majeruhi hao, alimwambia mwandishi wetu: “Hali zao kwa kweli zinaendelea vizuri kiasi ila wanatia huruma sana. Unajua kisaikolojia itawaathiri kwa muda mrefu kidogo. Tatizo hili limesababishwa na ujenzi wa kimagumashi.”
WAZIRI ANENAHali za majeruhi watatu ambao ni Jackson John (26) mkazi wa Msingini, Ali Saleh Ali (35) mkazi wa Michakaeni na Yohana Richard (25) mkazi wa Machomanne zinaendelea vizuri.
Juma Ahmed, mkazi wa Chake Chake ambaye alifika hospitalini hapo kuwajulia hali majeruhi hao, alimwambia mwandishi wetu: “Hali zao kwa kweli zinaendelea vizuri kiasi ila wanatia huruma sana. Unajua kisaikolojia itawaathiri kwa muda mrefu kidogo. Tatizo hili limesababishwa na ujenzi wa kimagumashi.”
Akitoa tamko la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, aliwataka wananchi waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwao.
“Nimepokea habari hii kutoka kwa viongozi wenzangu na kwa kweli imenisikitisha sana. Sisi kama serikali tunatoa pole kwa wafiwa na kuwatakia afya njema waliojeruhiwa ila nawataka ndugu kuwa na subira katika tukio hili,” alisema
Chanzo ni gazeti la Uwazi.
No comments:
Post a Comment