WALIOMTEKA NYARA ASKOFU WASAKWA NIGERIA
Polisi nchini Nigeria wanawasaka
wanaume waliomteka nyara kiongozi wa ngazi ya pili wa kanisa la
kianglikana nchini Nigeria Askofu mkuu Ignatius Kattey.
Askofu Ignatius ni mkuu wa kanisa la kianglikana tawi la jimbo la Niger Delta.
Alitekwa nyara Ijumaa jioni akiwa na mkewe Beatrice, karibu na makao yao mjini Port Harcourt, Kusini mwa nchi.(P.T)

Katika miaka ya hivi karibuni, visa
vya watu kuteka nyara wakati wakidai kulipwa kikombozi vimekuwa jambo la
kawaida katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta
linalozingira Port Harcourt
Mwaka jana mamake waziri wa fedha, Ngozi Okonjo-Iweala alitekwa nyara na kuzuiliwa kwa siku tano.
Hakuna kundi lolote limedai kumkamta Askofu huyo akiwa na mkewe.
Makundi mengi ya magenge ya watu waliojihami, huendesha shughuli zao katika eneo hilo kutokana na miaka mingi ya migogoro katika eneo hilo dhidi ya sekta ya mafuta.

No comments:
Post a Comment