NJAMA YA FIFA KUHUJUMU QATAR
Kamati andalizi ya Kombe la dunia la
mwaka wa 2022 itakayokuwa Qatar imekatalia mbali pendekezo la shirikisho
la soka duniani FIFA ya kupeana mashindano hayo kwa taifa lingine.
FIFA imependekeza kuhamisha
kidumbwedumbwe hicho hadi msimu wa baridi ili kuepuka viwango vya juu
vya joto kama inavyo shuhudiwa katika mataifa ya Ghuba.(P.T)
Viwango vya joto huwa vinapanda hadi nyuzi joto 40 C.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la
Uingereza Greg Dyke amesema iwapo hakutakuwa na makubaliano ya
kubadilisha saa za kuandaa mechi za kombe la dunia basi hakutakuwa budi
ila kubadili uwenyeji wa kombe la dunia.
Hata hivyo Katibu wa kamati andalizi
ya mashindano hayo ya QATAR 2022 Hassan al Thawadi amekatalia mbali hoja
hiyo akisisitiza Qatar ilishinda fursa hiyo ya kuandaa kombe la dunia
la mwaka 2022 na ni sharti watimize azma yao.
''Tulijitahidi kunadi muundo msingi
wetu na tukafaulu kuwa mwenyeji wa kombe la dunia tukizingatia sera na
mifumo ya FIFA itakuwaje sasa inasemekana kuwa tulikosea ''
Mwenyekiti huyo alifoka baada ya Rais
wa FIFA Sepp Blatter Kuduwaza ulimwengu kwa kukukiri kuwa Shirikisho la
FIFA Lilikosea kuteua Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka wa
2022.
Qatar ilizipiku Korea Kusini, Japan Australia na Marekani iliposhinda uwenyeji wa mashindano hayo
No comments:
Post a Comment