Joseph Kaniki anaswa na madawa ya kulevya Ethiopia....
Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya
Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni
wakituhimiwa kwa makosa hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya
Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward
kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa
kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya
Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya
Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa
doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa
na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za
Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda
ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea
Paris, Ufaransa.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Samuel
Shelukindo alithibitisha jana kwamba wanamichezo hao wanashikiliwa
nchini humo na Polisi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai.
Wanamichezo hao wamepandishwa kizimbani katika
Mahakamu Kuu ya Ethiopia iliyoko kwenye eneo la Arada, Addis Ababa
kujibu tuhuma za kubeba kilo saba za dawa hizo haramu.
Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Mkwanda anadaiwa kubeba kilo nne wakati Kaniki akidaiwa kubeba kilo tatu. Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufungwa kifungo cha miaka tisa hadi 15.
Alisema uwezekano wa kesi ya Kaniki na Matumla
kurudishwa Tanzania haupo kwa kuwa nchi hizi mbili hazina utaratibu wa
kubadilishana wafungwa.
“Wameshikiliwa hapa Ethiopia kwa zaidi ya siku 10
sasa, sisi tulipigiwa simu na polisi wa hapa Alhamisi iliyopita
kujulishwa kwamba kuna Watanzania wawili wameshikiliwa kwa tuhuma za
kukutwa na dawa za kulevya, tulipokwenda tukamkuta ni Kaniki na
Matumla,” alisema Shelukindo.
“Wao wenyewe wanaeleza kwamba walipitia Mombasa na
huo mzigo walipewa na mtu mmoja. Lakini Kaniki yeye anajitetea kwamba
huyo aliyewapa huo mzigo pale Mombasa anajuana vizuri na Mkwanda.
“Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe.
"Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Kwa hiyo alichofanya yeye ni kuubeba tu. Walikuwa wapitie hapa Addis wakashuke Paris, Ufaransa ndipo warudi Sweden kwa njia zao wanazojua wenyewe.
"Walipofika hapa Mkwanda alifanikiwa kupenya akapanda ndege lakini Kaniki akanaswa na mbwa ndipo akajitetea kwa polisi kwamba lile begi lilikuwa lake lakini mizigo mingine ilikuwa ya Mkwanda.
“Ndipo hapo sasa Mkwanda akashushwa kwenye ndege
wakashikiliwa na Jumatatu ya wiki iliyopita wakapandishwa kwenye
Mahakama ya hapa kutajiwa kesi yao lakini hawakupewa nafasi ya
kujitetea. Kesi itatajwa tena Jumanne (leo) na Jumatano (kesho) na
uchunguzi wa polisi bado unaendelea.”
Wanamichezo hao walidai kwamba walikabidhiwa
mizigo hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa walipokuwa wakikabidhiwa
pasi za kupandia ndege baada ya kupita sehemu zote za ukaguzi
“Kilichotokea ni jambo la aibu kwa nchi na hata wachezaji
wenyewe wanajuta. Kwa mfano, Kaniki anasema alikuwa aende England
kucheza mpira Desemba lakini sisi tukamwambia hatuwezi kumsaidia inabidi
akabiliane na kesi iliyoko mbele yake.
"Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.
"Mkwanda yeye ametuambia kwamba anaishi Sweden hatuna maelezo yake zaidi,” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa wamewapelekea wanamichezo hao msaada wa mablanketi kwa vile bado wako mahabusu na Ethiopia kwa sasa kuna baridi kali.
Shelukindo alisema wachezaji hao wapo mahabusu
kwenye Kituo cha Polisi cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (Federal Police
Crime Investigation) na hawana chochote zaidi ya nguo walizokuwa
wamevaa.
Watanzania wengine kuachiwa leo
Shelukindo alisema kuna Watanzania wanne
wanaotazamiwa kuachia leo baada ya kumaliza vifungo vyao baada ya
kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
“Kuna Watanzania wengine walinaswa hapa miaka ya
nyuma wao walikuwa wamemeza wakapasuliwa dawa zikatolewa na baadhi yao
walifariki. Hata hivyo, wanne ambao wamemaliza vifungo vyao vya miaka
minne wanaweza kurudishwa Tanzania,” alisema Shelukindo.
-Mwananchi
-Mwananchi
No comments:
Post a Comment