ABASI TARIMBA NA MWENYEKITI WA MTAA WA HANANASIFU WAMKACHA ASHA BARAKA ZOEZI LA UBOMOAJI
Mkurugenzi
wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec
CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza na mtandao huu jana jioni
alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na
vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka
kwa mazungumzo na wahusika:CHANZO MUHIDIN SUFIAN
Zoezi
hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu
mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya
mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa
kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.
Baada ya
alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba
zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji,
lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha
eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo
hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.
Aidha
baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu
za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na
walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji
utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili
kuendelea na biashara.
Cha
kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa
kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi
wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa
taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani
Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili
kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.
Lakini
cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani,
jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.
Wakati wa
zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini
naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya
mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa
kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.
Hata
hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao
kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa
ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni
kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta
wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
No comments:
Post a Comment