SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA
SEMINA
kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) kwa waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka
kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu)
katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.
Mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti
14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na
Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza
kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde. (HM)
Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.
Chanzo: Boniface Wambura

No comments:
Post a Comment