MAN UNITED NA CHELSEA ZATOKA SARE YA 0-0
Rooney akimdhibiti Ramires
KOCHA wa
Manchester United, David Moyes amepeleka ujumbe kwa Chelsea kwamba Wayne
Rooney hatahamia Stamford Bridge majira haya ya joto kufuatia mchezo wa
usiku huu wa miamba hao uliomalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye
Uwanja wa Old Trafford.
Rooney alianza katika kikosi cha
kwanza baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba
atajiunga na Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya
uhakika leo akiwa na uzi mwekundu.
Chelsea ilianza bila washambuliaji
wake Fernando Torres na Romelu Lukaku walioanzia benchi, lakini gumzo
zaidi ni kila upande kulalamikia kunyimwa penalti katika mechi hiyo.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie. Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie. Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'.
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka
kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti
na hata Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo mzuri.
Jose Mourinho alisema baada ya mechi
mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo,
wakati Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na
kuwapongeza vijana wake kwa soka nzuri.
Kikosi cha Man United kilikuwa: De
Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia/Young dk67, Cleverley,
Carrick, Welbeck/Giggs dk78, Rooney na Van Persie.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill,
Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne/Torres dk60, Oscar,
Hazard/Azpilicueta dk93 na Schurrle.
No comments:
Post a Comment