MWAKYEMBE AWASHUKIA WAPELELEZI DAWA ZA KULEVYA
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewashukia waendesha mashitaka na
wapelelezi kesi zinazohusiana na dawa za kulevya kuwa hadi sasa
zimefikia 36 lakini hakuna taarifa zake.
Mwakyembe
aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye Kipindi cha Jenerali On Monday
kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten juzi usiku.
hdg
Mwananchi
iliwasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka, Elieza Feleshi kuhusiana na
hilo, lakini hata hivyo simu yake ilikuwa haipatikani. Hata ilipofika
ofisini kwake, ilielezwa kuwa alikuwa kwenye mkutano.
Kamanda
wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alipotafutwa jana
kuzungumzia hali hiyo, simu yake ilikuwa haipatikani.
"Kila
anayekamatwa lazima achukuliwe hatua stahiki kwa kosa lake na hakuna
sababu ya kuleana wala kuogopana," alisema Dk Mwakyembe ambaye
ametangaza kujitoa muhanga kupambana na mtandao wa dawa za kulevya
nchini.
Mwakyembe
aliyekuwa akizungumzia mapambano hayo aliyoyaanzisha ya dawa za
kulevya, alirejea sakata la kuvushwa dawa za kulevya Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere, JNIA alisema: "Wote tumewafukuza kazi kwa sababu
walihusika kupitisha dawa hizo."
Hata
hivyo, Mkurungenzi wa JNIA, Moses Malaki akizungumza na gazeti hili,
alisema juzi kuwa utaratibu wa kuwapatia barua zao umekamilika na sasa
kinachofuata ni utaratibu wa kuunda tume ambao utafanyika wakati wowote
kwa ajili ya uchunguzi na kuwahoji.
Wafanyakazi hao wa JNIA, wanatuhumiwa kula njama za kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.
Dk
Mwakyembe alisema pia kuwa watu hao watafukuzwa kazi pamoja na wahusika
wengine. "Ule mkanda unaonyesha watu walivyokuwa wakihangaika siku ile
pale. Kuna askari anaonekana anasaidia kupitisha mizigo kwenye mashine,
huyu askari ni kazi yake hii?
"Wapo
watu walikuwa wakihangaika huku na huko, yaani walikuwa hawatulii, ni
kama sinema, wengine wako 'bize' na simu badala ya kufanya ukaguzi, sasa
tumewafukuza...Najua wapo wengine, nasema kama mtu aliona, alisikia na
hakusema naye atakwenda na maji.
Alisema
amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili
ya kufanikisha kazi hiyo. "Nimemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani tufanye
kazi na lazima tuumalize huu mtandao."
Akizungumzia
ukaguzi wa mizigo, Dk Mwakyembe alisema lazima mizigo yote ikaguliwe
hata bandarini. "Pale Uwanja wa Ndege kuna mitambo pengine bora zaidi
kuliko mahala pengine popote Afrika na kama haitoshi, tuongeze mingine
zaidi.Alipoulizwa kama atakuwa na ubavu wa kuzuia 'unga' wa vigogo,
Mwakyembe alisema: "Kigogo yeyote atakayejitokeza nitamkamata
tu...Ajitokeze sasa hivi aone. Nimeshangazwa na kilo 180 kupita, huu
mtandao wa kipuuzi lazima kuuvunja.
"Asije
mtu akatarajia kuchekewa, ataondoka. Atakayeruhusu mtu kupita na dawa za
kulevya, tukibaini, ataondoka tu. Wako wengi wanatafuta kazi.
Tulijiachia vya kutosha, na sasa basi."
Akizungumzia
hali ilivyo Bandarini kwa sasa, alisema wameimarisha udhibiti wa
upotevu wa makontena. "Hali kwa sasa ni nzuri, ilikuwa aibu, kila siku
makontena yanapotea, tulianzisha utaratibu, kontena likipotea kitengo
kizima wanakatwa mishahara kulipia," alisema.
Alisema pia kumeanzishwa utaratibu wa kukagua mizigo yote inayoingia na kutoka.CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment