CAG ADAI KWAMBA MAGUFULI SIYO FISADI.....ATOA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU ZILE BIL. 252
 MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema taarifa ya Sh bilioni 252 zilizokuwa zimeoneshwa katika taarifa ya Wizara ya Ujenzi, zilihamishwa kwenda Wakala wa Barabara (Tanroads) kulipia madeni ya wakandarasi na kwamba hapakuwa na ufisadi.
Akizungumza
 na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Utouh alisema vyombo vya 
habari viliripoti suala hilo tofauti, baada ya Kamati ya Hesabu za 
Serikali (PAC) kukutana na wizara na kuhoji juu ya matumizi ya fedha 
hizo.
Utouh
 alisema baada ya PAC na Kamati ya Kudumu ya Serikali za Mitaa (LAAC) 
kupitia ripoti ya Wizara ya Ujenzi, kumejitokeza upotoshaji wa taarifa 
kuhusu hesabu za wizara hiyo na taarifa zisizo sahihi, zikidai kulikuwa 
na ufisadi.
Alisema
 fedha hizo zimeoneshwa kwenye taarifa ya hesabu za Wizara hiyo, kama 
vile ni miradi mipya ya mwaka 2011/2012 tofauti na uhalisia wake.
Utouh
 alisema uhalisia wa fedha hizo ni kuwa mara baada ya kupokewa na Wizara
 ya Ujenzi kutoka Hazina, zilihamishwa kwenda Tanroads kulipia madeni ya
 wakandarasi wa miradi ya barabara, iliyotekelezwa na wahandisi 
washauri, ambao walikuwa hawajalipwa kwenye mwaka wa fedha 2010/2011.
“Fedha
 hizi zilijumuishwa kimakosa kwenye hesabu za Wizara kama matumizi ya 
akaunti ya maendeleo, hivyo kuongeza matumizi ya Wizara kimakosa kwa 
kiasi hicho. 
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Kihasibu fedha hizo zilipaswa kuoneshwa kwenye hesabu za mtumiaji halisi wa fedha ambaye ni Tanroads na siyo Wizara hiyo,” alisema Utouh.
Alisema
 kutokana na hali hiyo, hesabu za wizara hazikuwa sahihi, kutokana na 
uwepo wa ongezeko hilo kubwa la fedha na hivyo kusababisha kupewa hati 
ya ukaguzi yenye mashaka.
“Hivyo
 katika kujadili hesabu za Wizara ya Ujenzi hakukuwepo na tuhuma zozote 
za ufisadi, ila Kamati ya PAC ilimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa 
Hesabu za Serikali kuihakikishia matumizi ya fedha hizo, jambo ambalo 
tumejiridhisha nalo kwa ushahidi wa namna mlolongo wake ulivyo hadi 
zilipotumika” aliongeza Utouh.
Aidha,
 alisema mbali na dosari hiyo ya kihasibu, Wizara ya Ujenzi inafanya 
kazi nzuri ya kusimamia na kujenga barabara katika kona zote za nchi, 
hivyo viongozi wake wanapaswa kupongezwa kwa kazi hiyo wanayoifanya huku
 akiwataka kuwa na moyo wa kuchapa kazi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya 
taifa.
Katika
 hatua nyingine, Utouh alimpongeza Spika wa Bunge Anne Makinda kwa 
uamuzi wake wa kupanga upya Kamati za Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu 
(PAC), kwa madai kuwa utasaidia kuleta ufanisi na tija katika utendaji 
kazi wa kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment