TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, August 22, 2013

MUGABE KUAPISHWA LEO ZIMBABWE

Pope6_04397.jpg
Sherehe za kuapishwa kwake zimekuwa zikicheleweshwa kwa sababu ya kesi iliyokuwa imewasilishwa mahakamani kupinga kuchaguliwa kwake na mpinzani wake mkuu Morgan Tsvangirai , ambaye alidai kulikuwa na wizi wa kura.Tsvangirai pia anadai wapiga kura wake milioni waliondolewa kwenye vituo vya kupigia kura katika maeneo ya mijini , yanayoaminiwa kuwa ngome yake ya kisiasa.
P.T

Itakuwa ni fursa nyingine kwa rais Robert Mugabe kutoa hotuba zake zenye makali hususan kuyashutumu mataifa ya magaribi kutokana na vikwazo vilivyowekewa zimbabwe na kuuponda upinzani unaoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu Morgan Changirai.
Ni nafuu iliyoeje kwa bwana Mugabe ambaye alilazimika kugawana madaraka na bwana Changirai kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kufahamu kuwa mara hii atakuwa ni yeye pekee kwenye usukani wa kuiongoza zimbabwe.
Zaidi ya marais arobaini wa mataifa ya kigeni wamealikwa katika sherehe za leo lakini haijabainika ni wangapi watahudhuria kushuhudia kuapishwa kwa Robert Mugabe katika uwanja mkubwa zaidi wa michezo nchini Zimbabwe mjini Harare. Leo Alhamisi imetangazwa kuwa siku ya alhamisi ili kuwaruhusu wafuasi wa rais huyo mkongwe kuhudhuria sherehe hizo.
Waandalizi wamesema kuwa sherehe za leo zinatarajiwa kuwa za hali ya juu kuliko sherehe za mwaka 1980 baada ya Zimbabwe kunyakuwa uhuru.
Hatua hii inalenga kuwashawishi raia kwamba uchaguzi uliofanyika ulikuwa wa haki baada ya shutuma kwamba kulikuwa na udanganyifu na wizi wa kura.
Mpinzani mkuu wa bwana Mugabe Morgan Tsvangirai alipuuzilia mbali uchaguzi huo, akiutaja kuwa bandia na ambao haukuashirii matakwa ya watu wa Zimbabwe. Bwana Changirai ametaka kufanyiwa ukaguzi daftari la kudumu la wapiga kura.
Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe ilitangaza kuwa chama cha Zanu PF kilishinda thuluthi tatu ya idadi ya viti bungeni na kwamba Mugabe alinyakuwa ushindi wa zaidi ya asilimia sitini ya kura zilizopigwa. Chama cha MDC chake Morgan Changirai kimesema kuwa hatahudhuria sherehe za leo.

No comments:

Post a Comment