SAMUEL ETO'O ATAMBULISHWA RASMI CHELSEA
Chelsea imemsajili mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o kutoka klabu ya Anzi Makhachkala ya Urussi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini na miwili amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Chelsea.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho,
aliamua kumsajili Eto'o baada ya maombi yake ya kumsajili nyota wa
Manchester United Wayne Rooney kukataliwa.(P.T)
Mapema
wiki hii, ilibainika kuwa Rooney hakuwa tayari kulazimisha uhamisho wake
kwa kuwasilisha ombi lake la kutaka kuondoka na hivyo kuzima matumaini
ya Chelsea ya Kumsajili mchezaji huyo.
Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara
nne wa mchezaji bora wa soka barani Afrika, alikuwa nyota wa AC Milan
mwaka wa 2010 wakati Mourinho alipoiongoza kushinda kombe la klabu
bingwa barani Ulaya.
Mwaka wa 2011, Eto'o alivunja rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.
Klabu hiyo ya Anzi pia imemuuza kiungo
wake Willian, mwenye umri wa miaka 25 kwa klabu ya Chelsea, baada ya
mmiliki wa klabu hiyo mfanya biashara tajii Suleyman Kerimov kupunguza
bajeti ya klabu hiyo.
Eto'o
alianza kucheza soka ya kulipwa na klabu ya Real Madrid, lakini
alisajiliwa na vilabu vya Leganes na Real Mollorca kwa mkopo kabla ya
kupata mkataba wa kudumu Mallorca mwaka wa tisini na tisa.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa katika
kikosi cha Cameroon kilichoshinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka wa
2002, vile vile alishinda kombe la Copa del Rey, kabla ya kujiunga na
klabu ya Barcelona mwaka wa 2004.
Akiwa katika uwanja wa Nou Camp,
alishinda kombe la klabu bingwa barani ulaya mara mbili mwaka wa 2006 na
2009 na alifunga bao katika fainali hizo mbili pamoja na kushinda kombe
la ligi kuu ya La Liga mara tatu.
Mwaka wa 20098, Barcelona iliilipa
Inter Milan pauni milioni arubaini pamoja na mchezaji huyo ili kumsajili
Zlatan Ibrahimovic na mshambuliaji huyo alifanikiwa kushinda kombe la
klabu bingwa barani Ulaya kwa mara nyingine chini ya Uongozi wa Mourinho
katika uwanja wa San Siro.
Alijiunga na klabu ya Anzi na ripoti zinasema kuwa alikuwa akilipwa £167,825 kwa wiki mwaka wa 2011.
No comments:
Post a Comment