YANGA, AZAM KUVAANA NGAO YA JAMII J’MOSI
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi)
kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa
msimu mpya wa 2013/2014
Mechi
hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini
itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo
mshindi atakabidhiwa ngao.
Iwapo
dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa
mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda
kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na
bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti
vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A
watalipa sh. 30,000.
LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA SEPT 14
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa
katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi
Septemba 14 mwaka huu.
Kila timu
itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili
(nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.
Mechi za
ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors (Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni Transit Camp
vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends Rangers
(Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon
itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B
ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba
Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale
JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC
vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi za
ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume,
Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika,
Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na
Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Mzunguko
wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili
utamalizika Machi 22 mwakani. (Ratiba imeambatanishwa)
No comments:
Post a Comment