SERIKALI YAINGILIA KATI SAKATA LA YANGA ,AZAM TV
Sakata la Yanga kugomea udhamini wa
Azam TV limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Vijana, Habari Utamaduni
na Michezo, Dk Fennela Mukangara kuomba kukutana pamoja na Yanga, Azam
na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Katika taarifa yake
aliyoitoa jana, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Amos Makala alisema Waziri
Mukangara ameagiza kukutana na pande zote Agosti 14, kabla ya Ligi Kuu
kuanza.
Yanga walipeleka barua ya malalamiko
kwa Waziri Mukangara ya kugomea udhamini wa Azam TV kwa kile walichodai
kulazimishwa kukubali mkataba...(HM)
huo na kwamba hawajakurupuka kufanya
uamuzi wao wa kugomea Azam TV kwani wamefanya uchambuzi wa kina juu ya
makubalino ya kibiashara ya Bodi ya Ligi (TPL) na Azam TV na wametambua
hauna masilahi na klabu yao na ndiyo maana wamegomea mechi zao kurushwa
na Azam TV.
Hata hivyo,Lakini katika maelekezo yake Dk Mukangara kwa nNaibu wake Makala alisema, "N"nimeongea na wadau wa soka na narejea barua ya Yanga kwa wWaziri, nafikiri kuna haja ya Serikali kuingilia suala hili kwa kukutanisha pande zote kabla lLigi haijaanza, nakuelekeza kwa maelekezo yangu uwawandikie ombi la kuwa na kikao cha pamoja kati ya viongozi wa Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Azam."
"Kikao kitakuwa Agosti 14 saa tano kamili tulizungumze suala hili kwa masilahi ya soka la Tanzania na ili kuwa na uelewa mzuri wa jambo hili nashauri kila upande uwe na wanasheria wa taasisi zao," alisema Mukangara na kuagiza hadi kufikia leo pande zote ziwe zimeshapata barua hizo za wito.
Tayari Yanga wameshaitisha mkutano wa dharura wa wanachama wao Agosti. Chanzo: mwananchi

No comments:
Post a Comment