TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, August 15, 2013

IDADI YA VIFO MISRI YAZIDI KUONGEZEKA

misri a4eba
Wengi wa waathiriwa walifariki dunia katika mji mkuu wa Cairo lakini kulikuwa na vurugu katika maeneo yote ya nchi katika siku iliyoshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu tangu mapinduzi ya kidemokrasia yaliyotokea miaka miwili iliyopita. (HM)

Idadi kamili inaaminika kuwa juu zaidi kwa kuwa miili mingi ya waliofariki dunia bado haijasajiliwa.
Wafuasi wa rais Mohammed Morsi, aliyeng'olewa marakani mwezi uliopita wanasema zaidi ya watu 2,000 waliuwawa.
Mwandishi wa BBC Khaled Ezzelarab ameripoti kuwa ameshuhudia zaidi ya miili 140 ikiwa imefungwa kwenye sanda katika Msikiti wa Eman, uliopo karibu na kambi ya maandamano ya Rabaa al-Adawiya.
Vugugu la Undugu wa Kiislamu, Muslim Brotherhood, ambalo linamuunga mkono bwana Morsi, linapanga maandamano mengine mjini Cairo na mji wa pili kwa ukubwa, Alexandria, kulalamikia mauaji hayo. Chanzo: bbcswahili

No comments:

Post a Comment