TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, August 27, 2013

MAREKANI:KEMIKALI ILITUMIKA KUUA SYRIA

 kerry_0d4b0.jpg

Waziri wa Mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, John Kerry ameshtumu anachokitaja kama hatua ya serikali kutumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake kama ukosefu wamaadili wa hali ya juu.
Amesema kanda za video za silaha zinazotuhumiwa kuwa za kemikali karibu na mji wa Damascus ni kweli na zisizoweza kukanushwa.
Kerry aliongezea kwamba Rais Barack Obama anatafakari hatua ya kuchukua.
Haya yanajiri saa chache baada ya wakaguzi wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa kushambuliwa karibu na mji mkuu huo.
Wachunguzi wa silaha za Umoja wa mataifa kuwasili katika eneo lililopo viungani mwa mji mkuu Damascus ambapo inashukiwa kuwa wiki iliyopita kulishambuliwa kwa silaha za kemikali .
Wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanasema wachunguzi hao wa Umoja wa mataifa wanakutana na waathiriwa wa shambulio linaloshukiwa kuwa ni la gesi ya sumu na madaktari waliowatibu .
Wachunguzi hao watachunguza mabaki na kukusanya sampuli za udongo, damu na tishu kwa ajili ya vipimo vya maabara. .
Awali watu wasiojulikana wenye silaha waliushambulia kwa risasi msafara wa magari waliokuwemo wakaguzi hao walipokuwa wakielekea kwenye eneo la tukio - na kuwalazimisha kurejea nyuma kwa muda .
Vyombo vya habari vya kitaifa nchini viliwashutumu waasi kufanya shambulio hilo.
Rais Assad aliwaruhusu wakaguzi wa silaha baada ya kukabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa, lakini Marekani na Uingereza zimesema ushahidi mwingi huenda uliharibiwa katika muda wa siku tano, tangu kutokea kwa mashambulio.
Wakati huo huo serikali za magharibi zimeikosoa Syria kwa kuchukua muda mrefu kuruhusu timu ya Umoja wa mataifa ya wakaguzi wa silaha kuzuru eneo linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha za kemikali na zinaangalia uwezekano kuingilia kati kijeshi nchini humo.
P.T

No comments:

Post a Comment