MAJANGA ARSENAL, PODOLSKI NJE SIKU 21, RAMSEY NA WILSHERE NAO WAUMIA
Aaron Ramsey aliondoka uwanjani kabla ya mwisho wa mechi kutokana na maumivu ya nyonga
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Lukas
Podolski ataukosa mchezo wa Jumapili wa wapinzani wa London Kaskazini,
dhidi ya Tottenham baada ya kuumia nyama katika mchezo wa Ligi ya
Mabinwa jana dhidi ya Fenerbahce.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa
Ujerymani anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki tatu baada ya kuumia
katika dakika za mwanzoni za kipindi cha pili kwenye ushindi wa 2-0
katika mchezo huo wa marudiani, hivyo timu yake kusonga mbele hatua ya
makundi kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Waturuki.
Kocha Arsene Wenger amesema: "Tmetugharimu mno kwa majeruhi hayo, kwa sababu tunampoteza Podolski.
Aaron Ramsey alifunga mabao yote
katika usiku huo Arsenal ikijikatia tiketi ya kucheza hatua ya makundi
ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 16 mfululizo.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa
Wales naye pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioumia, akitoka nje
kabla ya mwisho wa mchezo na kuiacha Gunners ikimalizia mechi na
wachezaji 10.
Kiungo Jack Wilshere pia naye alipatwa na misukosuko, alipokabiliana na Raul Mereiles na Bruno Alves, na kumuachia maumivu.
Wenger alisema: "Sifahamu kiasi gani
Ramsey ameumia. Sifahamu Wilshere anaendeleaje. Tutaangalia hiyo kesho
(leo) asubuhi. Makwanja mawili kwa Wilshere yalisikitisha, lakini
anaonekana yuko sawa.
"Jack atakuwa sawa Jumapili. Natumai
hivyo kwa Aaron pia. Nilimuona akitoka nje zikiwa zimesalia dakika tatu
au nne mechi kumalizika, lakini sijui anajisikia vibaya kiasi gani.
Alitaka kubaki uwanjani,".
Wenger alitaka kumtoa nje Wilshere,
kutokana na historia ya matatizo ya maumivu ya kifundo cha mguu kwa
mchezaji huyo, lakini mchezaji huyo akaamua kuendelea kucheza.
"Nilitaka kumtoa nje, ndiyo," Wenger alisema. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment