SERIKALI YAAMUA YANGA NA KAMATI YA LIGI KUPITIA UPYA MKATABA
Hatimaye mkutano ulioitishwa na
serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kusuluhisha
mgogoro wa mkataba wa mauzo ya haki za matangazo ya Television
uliowashirikisha kamati ya ligi kuu ya soka Tanzania bara, klabu ya
Yanga na Azam Media umemalizika hivi punde huku maamuzi kadhaa
yakifikiwa. (HM)
Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha
mtandao huu, klabu ya Yanga ni kama imeibuka kidedea kwenye madai yake
ya kupinga utaratibu mzima wa mkataba huo baina ya kamati ya ligi na
Azam Media.
Hii inakuja baada maamuzi ya mkutano huo kuamuru kwamba vipengele vya mkataba huo kupitiwa upya na klabu ya Yanga na Kamati ya Ligi na vile ambavyo vitaonekana kuwa na matatizo virekebishwe.
Pia imeamuliwa kwamba Yanga SC itakaa kikao na Azam Media kuzungumzia mambo mbalimbali ambayo Yanga imeonekana kuwa na shaka nayo kuhusu Azam pamoja na maslahi ya Yanga kupitia dili hilo la ununuaji wa haki za matangazo ya TV ya mechi za ligi uliofanywa na Azam Media.

No comments:
Post a Comment