TSVANGIRAI ATUHUMIWA KUDHARAU MAHAKAMA
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe,
Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia
matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu
amesema waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya
yanajiri wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change
kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
P.T
Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njiya huru na haki. Mugabe alipata asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba kikisema hakikua imani ya kupata haki.
No comments:
Post a Comment